News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » MWANASHERIA WA OKWI ATAKA MKATABA WAKE UVUNJWE



UVUMILIVU umetushinda. Mwanasheria wa straika wa Yanga, Emmanuel Okwi, Dennis Aggaba amesema wikiendi hii atazungumza na mteja wake kujua kama amelipwa fedha zake zilizobaki za usajili au vinginevyo aanze mchakato wa kuvunja mkataba wake.
Desemba mwaka jana Okwi alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga kwa dau la dola 100,000 ambazo ni zaidi ya Sh. 159 milioni lakini hadi sasa amelipwa nusu ya fedha hizo na ameigomea timu hiyo hata kufanya mazoezi.
Akizunguma na Mwanaspoti kutoka Uganda, Aggaba alisema, kama Yanga watakuwa hawajamlipa Okwi hadi kesho Jumapili saa sita usiku, kuanzia Jumatatu ataanza mchakato wa kuvunja mkataba wa Yanga na mteja wake ambaye ni Okwi.
“Nilikuwa na kazi nyingi sana nikashindwa kumtafuta Okwi, lakini nitamtafuta kesho (leo Jumamosi) au Jumapili (kesho) ili nijue kama amelipwa fedha zake au bado, na hata haki zake nyingine za mkataba. Akiniambia bado hajalipwa, Jumatatu nitaanza mchakato wa kuvunja mkataba wake na kumrudisha SC Villa ambao bado wanamhitaji hadi sasa,” alisema Aggaba.
Tayari kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amepiga hesabu na kuchukua uamuzi wa kumuondoa Okwi katika kikosi chake kitakachocheza na Oljoro JKT kesho Jumapili na kumtaka amalize matatizo yake na uongozi haraka kabla ya wiki ijayo.
Okwi kwa sasa hayupo katika kikosi cha Yanga huku baadhi ya watendaji wa Yanga wakipanga sababu za kukacha mazoezi ya timu hiyo, japokuwa Mwanaspoti linafahamu kuwa kiasi cha fedha za usajili ambacho hajamaliziwa ndiyo sababu kuu.
Katibu wa Yanga, Beno Njovu alisema Okwi ni majeruhi ndiyo maana haonekani katika mazoezi ya timu hiyo, lakini daktrari wa timu hiyo, Juma Sufiani alisema: “Sina taarifa za kuumwa kwa Okwi, kutokuwepo kwake katika timu ni matatizo yake na uongozi.”.
Akizungumza na Mwanaspoti, Pluijm alisema “Okwi nimemwacha nimeondoka na wachezaji 24 walio sawa kimchezo, nimemueleza sababu za kuamua kumuach ana nimemtaka kukutana na uongozi ili amalize matatizo yake na uongozi.”
Source Mwanaspoti.



Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu