Desktop

Chat

Bookmarks

User

Mail

Videos

Contact

Mobile

Archive

News

Music

Makala

Sokkaa

Video

DART YAKANUSHA TAARIFA POTOFU KUHUSU MABASI YAENDAYO HARAKA DAR



Kuna upotoshaji wa makusudi uliozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mabasi yaliyozinduliwa tarehe 17/08/2015 kuwa.
1. Ati ni ya Kichina

2. Milango ya kushukia na kupandia abiria iko kushoto hivyo hayaendani na miundombinu iliyojengwa.
HUO NI UZUSHI WENYE LENGO LA KUWAPOTOSHA WATANZANI WALIOCHOSHWA NA MSONGAMANO UNAOONGEZEKA SIKU HADI SIKU
TAARIFA SAHIHI KUTOKA KWENYE MAMLAKA HUSIKA HII HAPA:
1. Kiwanda kilicho assemble (Kuunganisha) mabasi haya kinaitwa Golden Dragon cha China.
2. Aina ya injini ni CUMMINS ya Marekani (USA)

3. Aina ya giaboksi ni VOITH ya Ujerumani.

4. Mfumo wa stelingi ni ZF ya Ujerumani.

5. Mgumo wa difu ni kutoka Marekani (USA).

6. Aina ya suspension (za upepo) Air Suspension kutoka Marekani (USA).

7. Mfumo wa breki ni WABCO

8. Aina za mabasi ziko mbili. Articulated mita kumi na nane almaarufu (Ikarusi) kutoka Hungary zitakazopita kwenye barabara Maalumu za zege zilizojengwa na Mabaai ya mita kumi na mbili yanayoitwa (Feeder) Mabasi Mlisho yatakayotumia vituo vilivyoko nje ya mfumo mfano kituo cha Shekilango, Morocco Hotel, Mwanamboka na Magomeni Mapipa kuwapeleka na kuwaleta kwenye mfumo.

9. Milango ya kupanda na kushukia abiria ipo kulia na kushoto ili kukidhi mahitaji ndani na nje ya mfumo ambayo idadi yake ni minne kila upande ila itatumika mitatu na mmoja niwa dharula kila upande.

10. Urefu kutoka ardhini kwa milango ya kushoto ya basi ni sentimita thelathini (30) ambayo hata mtoto anaweza kushuka bila msaada wa mtu mzima.

11. Urefu wa milango ya kulia ni sentimita tisini (90) sawa na urefu wa platform za kila kituo cha DART unaomuwezesha hata mtu mwenye mahitaji maalum Kuingia na kutoka ndani ya basi bila msaada wa mtu.

12. Ndani ya basi kuna eneo la kukaa watu wenye mahitaji maalum - walemavu, wazee na mama wajawazito.

13. Mfumo wa ulipaji nauli unafanyika vituoni kama ilivyo kwenye kivuko pale Kivukoni hivyo basi hili halina Kondokta. Makondakta wapo vituoni.

14. Muda wa safari kutoka Kivukoni hadi Kimara ni wastani wa dakika thelathini (30) ikihusisha muda wa kushusha na kupakia kwenye vituo vya DART.

15. Ni marufuku kwa chombo ama mwananchi kutumia barabara maalum za mabasi. Wananchi watumie maeneo yaliyotengwa maalum kulingana na mahitaji. Watumiaji wa bodaboda wanatakiwa kupita kwenye barabara zinazotumiwa na magari ya kawaida na siyo eneo lililotengwa kwa ajili ya watembea kwa miguu.
HIZI NDIZO TAARIFA MUBIMU NA RASMI KWA WATANZANIA

Baada ya baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie kuonesha msimamo wao katika kuwaunga mkono wagombea flani wa Urais.Ray aweka Msimamo wake!!



Msanii mwenzao Ray Kigosi ameonesha msimamo wake na kwa maneno haya.

''"Usiku wa jana nimetafakari vi2 vingi sana kuhusu Nchi yangu iliyobarikiwa kila aina ya utajiri wa madini mbuga za wanyama wakiwemo aina mbalimbali za wanyama wa kuvutia na hekta kubwa za misitu Ila ninaona vipofu wengi sana wasiolewa nini 2lichobarikiwa ndani ya Tanzania ye2. 
2meingizwa mikenge mingi sana katika mikataba tena mibovu bajeti kandamizi Kwa wa2 wa hali ya chini mifumuko ya bei kila kukicha hali ngumu kwa wasanii wa Tanzania kila siku ahadi zisizotekelekeza why nasema hivyo wasanii wenzangu?
 2meumia kwa kipindi kirefu sana bila msaada wowote ha2na haki miliki wa kazi ze2, zinaibiwa kama njugu sokoni kariakoo yani 2li2pwa kama taka taka kwenye dampo lakini sasa hivi kipindi cha uchaguzi ndio 2naonekana umuhimu we2 tuamke kuwaambia wananchi wachague viongozi makini watakaoweza ku2vusha Watanzania kwenda ha2a nyingine. 
Tuna wa2 wengi sana nyuma ye2 wanaotuamini sisi wasanii kama kioo cha jamii tusiwapoteze Watanzania kuwaambia Viongozi wa chama flani ndio wanafaa kwa vijisenti vidogo 2navyopewa. Watanzania huu ni wakati sahihi waku2lia na kuwachagua viongozi makini wanaofaa Ni katika kukumbushana 2 waswahili wanasemaje utakaokatanao kuni ndio utakaota nao moto.”''




Chadema yazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa



Uwanja wa Taifa 
By Julius Mathias
Dar es Salaam. Serikali imekataa ombi la Chadema la kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuzindua kampeni zake za uchaguzi, ikisema mazingira yaliyopo sasa hayaruhusu eneo hilo kutumika kwa shughuli za kisiasa.
Serikali imetangaza uamuzi huo ikiwa ni siku tatu kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani kwa ajili ya Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25.
Juzi, kwenye mitandao ya jamii kulienea habari kuwa Chadema, ambayo mgombea wake wa urais, Edward Lowassa amekuwa akivuta maelfu ya watu kwenye mikutano yake, imepanga kutumia uwanja huo unaoweza kuchukua watu 60,000 waliokaa kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni zake Agosti 22.
Hata hivyo, Chadema imeshakanusha taarifa kuwa itazindua kampeni zake Agosti 22.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Assah Mwambene alisema Serikali haijatoa ruhusa kwa chama chochote cha siasa kuutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya shughuli za kisiasa na kwamba hakuna chama kitakachoruhusiwa kufanya hivyo.
“Tulipata barua ya Chadema kuomba kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuzindua kampeni zao, tayari tumeshawaandikia kuwaarifu kuwa uwanja ule hauwezi kutumika kwa ajili ya shughuli zozote za kisiasa,” alisema Mwambene.
Alieleza kuwa Serikali imeamua kwamba uwanja huo uendelee kutumika kwa shughuli za kimichezo ili kuepuka mihemko na athari yoyote inayoweza kujitokeza kutokana na hamasa za kisiasa.
“Uamuzi huu unalenga kuweka uwanja katika mazingira rafiki ya michezo na kuepuka athari zozote zinazoweza kujitokeza,” alisema Mwambene.
Akizungumzia uamuzi huo, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema kilichofanywa na Serikali hakijaathiri chochote kwenye maandalizi ya harakati za chama hicho kufanya uzinduzi wa kishindo ili kukidhi matarajio ya Watanzania wanaokiunga mkono.
Alisema kilichotangazwa na Mwambene kimetokana na uelewa mdogo wa masuala ya demokrasia na masuala makubwa yenye mvuto wa kitaifa na kufafanua kuwa viwanja hivyo hutumika sehemu nyingi duniani kwa kuwa kampeni ni sehemu pekee ambayo wananchi wanapata nafasi ya kuwahoji wagombea kabla hawajawapa ridhaa ya kuwatumikia.
“Mwambene haelewi anachokisema. Anatumika kufunika aibu ya CCM ambayo imeona mvuto wake unaendelea kushuka kila siku. Hivyo hawana uhakika wa kujaza wafuasi kwenye eneo kubwa kama lile,” alisema.
“Kwa sasa ni Chadema pekee ndiyo inayoweza kuutumia uwanja ule, ndiyo maana CCM wamekimbilia viwanja vya Jangwani ambavyo kwa sasa ni vidogo kutokana na ujenzi wa vibanda vya biashara uliofanyika,” alisema Makene.
Alieleza kuwa CCM inatishwa na wingi wa watu wanaojitokeza kuiunga mkono Chadema baada ya kujionea maelfu ya watu wanaoambatana na mgombea wake wa urais hasa kwa kipindi cha kuomba udhamini mikoani.
“Tumekuwa tukiambatana na watu wengi sana ambao wamejitolea kuungana nasi kila tunapokwenda. Tunajipanga kufanya uzinduzi mkubwa eneo jingine na hii inaweza isifanyike Agosti 22, kila chama kinaweza kikaanza siku kinachoona inafaa kwake,” alisema.

Hizi ndizo Ahadi na Ilani Ya CCM



Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli na mgombea mwenza, Samia Saluhu Hassan 
By Beatrice Moses na Nuzulack Dausen
Dar es Salaam. Hatimaye Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeipua Ilani yake ya Uchaguzi kwa mwaka 2015-2020, ikitaja mambo makuu manne ya kushughulkikia katika miaka mitano ijayo, ambayo ni kupambana na umaskini, ajira kwa vijana, ulinzi na usalama na kupambana na rushwa kwa kuanzisha mahakama maalumu ya makosa hayo.
Ilani hiyo, iliyoandaliwa na makada wake 32 wakiongozwa na Stephen Wasira, imeanisha jinsi chama hicho kikongwe kilivyotekeleza baadhi ya ahadi zake katika ilani ya mwaka 2010-2015 na kutaja ahadi mpya zikiwamo zinazohusu ujenzi wa miundombinu, kukuza uchumi, viwanda, nishati, kilimo, sanaa na michezo pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama.
“Ilani hii ni tamko maalumu kwa wapigakura kuhusu nia ya CCM ya kuendelea kushika dola na kuwaongoza Watanzania kwa njia ya kidemokrasia na hasa kuendelea kudumisha amani, umoja wa kitaifa, usawa, ustawi wa wananchi, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kipindi kingine cha miaka mitano,” inasema ilani hiyo.
Kukamilika kwa ilani hiyo sasa kutamuweka huru mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli ambaye amekuwa akisita kumwaga sera kwenye mikutano ya hadhara kwa hofu ya kukiuka Sheria ya Uchaguzi na pia kutokuwapo kwa ilani hiyo.
Mkutano Mkuu wa CCM ulikuwa upitishe ilani hiyo Julai 12 mjini Dodoma, lakini mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete akaeleza kuwa ilikuwa katika hatua za mwisho za uhariri na kuomba chombo hicho kiridhie kazi hiyo kukamilishwa na Halmashauri Kuu.
Kwa mujibu wa ilani hiyo yenye kurasa 236, katika miaka mitano ijayo CCM itazielekeza Serikali zake za Muungano na Zanzibar kuboresha maisha ya wananchi wote na hususan vijijini, kwa kuchukua hatua mbalimbali ilizoziainisha, zikiwamo kukuza kilimo, miundombinu, viwanda, ajira na kupambana na rushwa.
Katika suala la rushwa, ilani hiyo imetaja mkakati wa mmoja wa makada walioomba kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho, Frederick Sumaye wa kuanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia matatizo ya rushwa.
Ilani hiyo inaeleza kuwa CCM itaimarisha “vyombo na taasisi zinazohusika katika kuzuia na kupambana na rushwa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mahakama maalumu kwa ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi”.
Mkakati huo umekuja wakati chama hicho kikikabiliwa na tuhuma za rushwa, hasa katika mchakato wa uchaguzi huku makada wake wakihusika katika kashfa zilizotikisa Taifa, hasa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyosababisha mawaziri wawili kuachia ngazi, sambamba na Mwanasheria Mkuu, wabunge na baadhi ya watendaji waandamizi wa Serikali.
CCM inaeleza katika ilani hiyo kuwa imedhamiria kukuza uchumi kwa miaka mitano ijayo kwa wastani wa asilimia nane au zaidi, kuinua ustawi wa Watanzania kwa kuongeza mapato ya wananchi kufikia kiwango cha wastani wa nchi ya uchumi wa kati, hivyo kuongeza fursa za ajira na kupunguza umaskini.
Ahadi nyingine katika kukuza uchumi ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei uendelee kubaki kwenye tarakimu moja, kudhibiti nakisi ya bajeti ili iendelee kushuka na kufikia kiwango kisichozidi asilimia tatu ya Pato la Taifa, pamoja na mambo mengine, Tanzania iendelee kupunguza gharama za kukopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Katika miundombinu, CCM imeendeleza ahadi za kujenga barabara, madaraja, vivuko, viwanja vya ndege, nyumba na majengo ya Serikali ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na huduma za jamii.
Hata hivyo, msisitizo wa ujenzi wa barabara umewekwa zaidi katika zile zinazounganisha Tanzania na nchi jirani, mikoa, na barabara zinazokwenda kwenye maeneo yenye fursa za kiuchumi kama Mchuchuma na Liganga na kujenga madaraja mapya ya Selander jijini hapa na Wami Chini la mkoani Pwani.
CCM imekusudia kuhamasisha kilimo kupitia kaulimbiu ya Kilimo Kwanza, kwa kuwawezesha wakulima kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa, pembejeo, zana za kisasa na wataalamu wa ugani pamoja na mbinu za kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao.
CCM inakusudia kuongeza kasi ya kupima ardhi na kuwapatia hatimiliki za kimila wananchi, ambazo watazitumia kama dhamana ya kuwawezesha kupata mikopo ya kuendeleza shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji na uvuvi.
“Kuendeleza na kuimarisha huduma za kijamii ikiwamo elimu, afya, maji, umeme na ujenzi wa nyumba bora pamoja na kuongeza kasi ya kurasimisha biashara kwa kuwapatia wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia biashara, leseni na fursa za kupata mikopo yenye masharti nafuu,” ilani hiyo inaeleza.
“Kuanza na kukamilisha ujenzi wa viwanja vya ndege vya Shinyanga, na Sumbawanga kwa kukarabati barabara za kutua na kuruka ndege, kujenga na kukamilisha awamu ya pili viwanja vya Tabora na Kigoma na kuanza ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Msalato kwa kiwango cha kimataifa,” inasema ilani hiyo.
Katika sekta ya afya, CCM imeahidi masuala mbalimbali ikiwamo kujenga hospitali tatu za rufaa kwa Kanda za Kusini, Kati na Magharibi na kuendelea kuimarisha zilizopo.
Iwapo itapatiwa ridhaa ya kushika dola, CCM imepanga kudahili wanafunzi 15,000 katika vyuo vya afya ifikapo 2020 kama jitihada kutosheleza mahitaji ya rasilimali watu na kuajiri wataalamu zaidi wa afya kutoka ndani na nje ya nchi kuboresha huduma za afya.
Ahadi nyingine ni kuimarisha upatikanaji wa dawa, huduma za mama na mtoto, kuimarisha huduma za matibabu ikiwamo kununua mashine za mionzi kwa ajili ya saratani na kuweka utaratibu wa wananchi kupata Bima ya Afya.
Kwa kutambua umuhimu wa ukuaji wa sekta ya mawasiliano, sayansi na teknolojia, CCM imeahidi kutenga kila mwaka kiasi kisichopungua asilimia moja ya pato ghafi la Taifa (GDP), kwa ajili ya utafiti, maendeleo na maonyesho.
Pia, kuwalinda watumiaji wa simu za mikononi dhidi ya uhalifu wa mitandaoni na kuongeza watumiaji wa intaneti kutoka milioni tisa mwaka huu hadi kufikia milioni 20 mwaka 2020.
Wakati baadhi ya wakosoaji wa masuala ya elimu wakieleza kuwa ubora wa elimu unapungua, CCM imekusudia kuhakikisha uandikishwaji wa rika lengwa la wanafunzi wa kidato cha kwanza unaongezeka kutoka asilimia 60 mwaka 2015 hadi asilimia 80 mwaka 2020... “Ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne utaongezeka kutoka wastani wa asilimia 69.8 mwaka 2015 hadi asilimia 90.0 mwaka 2020 na ufaulu wa daraja l hadi lll kutoa wastani wa asilimia 30.8 hadi asilimia 50.0.”
Credit Mwananchi

Pitia Kurasa Za mbele magazeti ya Leo Hapa










Hii ndiyo Fimbo ya kuwa Maliza Ukawa....Hatoki Mtu...



CCM kimepanga kuzindua kampeni zake za Uchaguzi Mkuu Dar es Salaam Jumapili. 

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza Kamati ya Kampeni yenye wajumbe 32, wengi wao wakiwa ni wale waliowahi kuvaana na mgombea wa Chadema, Edward Lowassa katika masuala tofauti.
Lowassa, Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, alijiondoa CCM mwishoni mwa mwezi uliopita na kujiunga na Chadema, ambayo ilimpa fursa ya kutimiza ndoto yake ya kugombea urais, akiwakilisha vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD.
Tangu ahamie Chadema, Lowassa amekuwa akivuta wafuasi wengi kwenye shughuli za Ukawa, hali inayoashiria uwezekano wa kuwapo kwa upinzani mkubwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Jana katika taarifa yake, CCM haikutoa maelezo mengi kuhusu kamati hiyo zaidi ya kutangaza kuwa itaongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana na kutaja majina ya wajumbe.
“Hii ni kamati ambayo itakuwa inafanya oparations za kila siku,” alisema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakati akitangaza kamati hiyo jana.
Kinana anajulikana kutokana na kazi aliyoifanya ya kuongoza kampeni kwa mafanikio, akifanikisha ushindi wa marais wawili mwaka 1995, wakati alipoongoza kampeni za Rais Benjamin Mkapa na 2005 wakati Rais Jakaya Kikwete akiingia Ikulu.
Licha ya Nape kutozungumzia majukumu ya kamati hiyo, mmoja wa wajumbe, January Makamba alisema wamejipanga vizuri na mwaka huu watafanya kampeni za kisasa.
“Tumejipanga na namna tunavyojipanga ni siri yetu, ni mambo ya ndani ambayo sisi wenyewe kwenye timu tunayafahamu na hatuwezi kutoa siri hizo kwa kuwa  ndizo silaha za maangamizi. Kwa kifupi tutashinda,” alisema naibu waziri huyo wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia.
Makamba, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, alisema kampeni za CCM mwaka huu zitakuwa za kisasa zinazoendana na mazingira ya kisiasa ya msimu huu.
“Tumejitayarisha kushinda, juhudi zetu na ari yetu ni kushinda na kampeni zetu zitakuwa za kisasa zaidi,” alisema Makamba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo alitumia mfano wa mpira wa miguu kuelezea ukubwa wa kamati hiyo dhidi ya wapinzani.
“Timu hiyo ya kampeni ni sawa na kuileta Arsenal kuja kucheza na timu ya daraja la tatu. Kwa hiyo katika hali hiyo usiulize matokeo,” alisema Bulembo ambaye alikuwa mdau wa soka kabla ya kuingia kwenye siasa.
Kamati hiyo ina wajumbe ambao walitemwa kwenye mbio za urais ndani ya CCM, wajumbe wa Kamati ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, wajumbe ambao walikuwa kambi ya Lowassa alipokuwa kwenye mbio za urais ndani ya chama hicho, wajumbe ambao ni maarufu kwa kurusha vijembe dhidi ya wapinzani na wajumbe ambao walishaweka bayana uhasimu wao na mbunge huyo wa Monduli.
Nape alisema Kinana atasaidiwa na makamu wenyeviti wawili ambao ni Rajabu Luhwavi (Bara) na Vuai Ali Vuai (Zanzibar) ambao pia ni manaibu wake kwenye chama.
Wajumbe ambao ni wale waliotemwa kwenye mbio za urais ni Dk Asha-Rose Migiro, Samuel Sitta, Mwigulu Nchemba, Dk Harrison Mwakyembe, Makamba, Lazaro Nyalandu, Stephen Wasira, Bernard Membe na Makongoro Nyerere.
Pamoja na kutopitishwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, makada hao wamekuwa wakieleza kuwa hawawezi kuhama chama kama alivyofanya Lowassa na watakuwa wakionyesha kuwa wamevunja makundi kwa kushiriki kumpigia kampeni Dk Magufuli.
Kamati hiyo pia inamjumuisha Sitta, Spika wa Bunge la Tisa ambaye anajulikana kwa kuruhusu mijadala dhidi ya Serikali. Katika mijadala hiyo, Bunge lliliunda kamati iliyoongozwa na Dk Mwakyembe kuchunguza sakata la Richmond lililosababisha Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu.
Katika hotuba yake ya kujiuzulu, Lowassa alidai kuwa suala hilo lilipikwa na mahasimu wake wa kisiasa kwa sababu ya uwaziri mkuu.
Kundi jingine la wajumbe wa kamati hiyo linahusisha makada waliokuwa kambi ya Lowassa alipokuwa anawania urais kupitia CCM lakini hawakuhama naye. Wajumbe hao ni Christopher ole Sendeka, Sadifa Juma Khamis, Shamsi Vuai Nahodha na Sofia Simba, ambaye alipinga uamuzi wa Kamati Kuu wa kupitisha majina matano na kuacha mengine kinyume na katiba.
Wajumbe wengine ni Livingstone Lusinde, Abdallah Bulembo na Nape, ambao wanajulikana kwa kushambulia wapinzani. Lusinde alijipatia umaarufu katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, Machi 2012 alipoamua kutumia lugha chafu dhidi ya viongozi wakuu wa Chadema.
Tayari Kinana, Mwigulu, Nape, Bulembo na Wasira wameshanukuliwa wakirusha mashambulizi makali dhidi ya Lowassa na wote waliohama CCM kuwa ni makapi na mafuta machafu na kwamba Magufuli atashinda.
Vilevile, wamo makada waliowahi kutangaza hadharani kuwa mahasimu wa Lowassa tangu alipokuwa ndani ya CCM, akiwamo Anthony Diallo. Kundi jingine ni la makada vijana kama Ummy Mwalimu, Steven Masele na Pindi Chana.
Wakizungumzia uteuzi huo, baadhi ya wajumbe waliishukuru CCM kwa kuwaweka kwenye kamati hiyo huku wakitamba kwamba watahakikisha chama hicho kinaendelea kuongoza nchi.
Mwalimu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, alisema uteuzi wake ni jambo linaloonyesha kuwa anaaminika na kuahidi kufanya kazi kwa juhudi kuhakikisha CCM inashinda.
“Kamati imejipanga,” alisema. “Kazi kubwa ni kuhakikisha Dk Magufuli anashinda na anaingia Ikulu kwa kuwa anauzika.
“Hatutishiwi na kitu, tunaamini katika kushinda na kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunashinda kwa kupambana. Magufuli anauzika.”
Ahadi ya kufanya kazi kwa bidii pia ilitolewa na Mbunge wa Kiembesamaki, Waride Bakari Jabu ambaye alisema atajituma kwa asilimia 100 kuhakikisha CCM inashinda.
“Nimefurahi na nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote kuhakikisha kuwa tunashika dola Zanzibar na Bara,” alisema.
Wakati Jabu akiyasema hayo, Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Maua Daftari alitaka wananchi wawaunge mkono katika kazi hiyo.
“Hili jukumu si la kwanza, lakini ninachoweza kusema ni kuwa wananchi watuunge mkono ili tushinde,” alisema na kusisitiza kuwa watahakikisha kampeni zinafanyika kwa usalama na wala si kwa fujo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo alisema amepokea uteuzi huo na anachosubiri ni kukaa na kupanga kitakachofanyika.
Makongoro, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), alisema hajapata taarifa rasmi kuhusu kuteuliwa kwake kwenye kamati hiyo.
Hata hivyo, alisema hiyo itakuwa ni mara yake ya pili kuwa kwenye kamati ya kampeni kwani aliwahi kufanya kazi kama hiyo alipokuwa NCCR-Mageuzi mwaka 1995. Alisema atazungumza zaidi kuhusu wajibu huo aliopewa pindi atakapopewa taarifa rasmi na Nape.
Wakati Diallo na Makongoro wakisubiri kikao, Nchemba, ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha, alitumia nafasi hiyo kumsifu Dk Magufuli.
“Sisi tunachokifanya ni kuweka njia tu ya kwa nini achaguliwe, kuwaambia Watanzania kwa nini anafaa, kwa kuwa awamu ya tano ni awamu ya kazi tu,” alisema.

Credit Mwananchi

Kipindupindu chaua mwingine Dar

 Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba Dar es Salaam, imeongezeka na kufikia watatu.
Mgonjwa wa tatu alipoteza maisha jana huku wengine wawili wakifariki dunia juzi. Hadi sasa wagonjwa 34 wamelazwa wakisubiri vipimo kujiridhisha kama wana ugonjwa huo.
Wagonjwa wanne waliokuwa wamelazwa kwenye Hospitali ya Mwananyama vipimo vyao vimeonyesha kuwa wana ugonjwa huo na wamehamishiwa kwenye kambi maalumu iliyoko katika hospitali hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema jana: “Tunachofanya ni kutoa elimu kwa wananchi kupitia mabwana na mabibi afya, ili kuhakikisha wagonjwa hawaongezeki, ikiwezekana kuzuia kabisa maambukizi mapya kwa namna yoyote ile.”
Makonda alisema ofisi yake inaboresha kambi iliyopo kwenye Kituo cha Sinza Palestina ili kuwaweka wagonjwa watakaogundulika kuwa na ugonjwa huo kutoka maeneo jirani na hapo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Aziz Msuya, alisema kambi maalumu kwa ajili ya wagonjwa hao ya Mburahati ipo tayari na wameshahamishia ikiwa tayari na wagonjwa 11 kutoka Mwananyamala.
Chanzo Mwananchi.

Hii ndiyo Kamati ya kampeni CCM 2015


Chama cha mapinduzi CCM kimetangaza wajumbe mahususi 23 kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu 2015 chini ya mwenyekiti Abdulrahman Kinana.

Rose Muhando aomba radhi!



Brighton Masalu
MWIMBAJI nyota wa nyimbo za Injili, Rose Muhando, amewaomba radhi watu wote aliowahi kuwakwaza, ikiwa ni pamoja na kuchukua fedha za kushiriki onesho, lakini akashindwa kufanya hivyo, akidai ni ubinadamu.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Rose alikiri kuingia baadhi ya mikataba na kushindwa kuitekeleza, akisema ni jambo lililomkosesha sana raha, hasa pale watu walipokuwa wakimchukulia kama tapeli.

“Hata hivyo, mara nyingi huwa nasingiziwa, lakini nakaa kimya kwa sababu nimeumbwa hivyo, kama kuna yeyote nimemdhulumu naomba anisamehe, sikufanya makusudi, nilishindwa kutokea kwa bahati mbaya, mimi ni binadamu. Namuomba pia baba yangu mlezi Msama (Alex, Meneja wake) naye kama kuna mahali nilimkwaza kwa matamshi au matendo, naomba anisamehe,” alisema nyota huyo wa kibao cha Facebook.

Chanzo GPL

Pata elimu kuhusu ugonjwa wa kuota vinyama sehemu za siri (Bawasiri, Hemorrhoids)


Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.


Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;


Tatizo sugu la kuharisha
Kupata kinyesi kigumu na kinyesi wakati mwengine kutokwa damu kisha ndio kupata kinyesi
Ujauzito
Uzito kupita kiasi (obesity)
Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
Umri mkubwa


Dalili za bawasiri


Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
Maumivu au usumbufu
Kinyesi kuvuja
Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa


Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri


Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
Strangulated hemorrhoids





Vipimo na uchunguzi


Digital rectal examination
Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)


Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri


Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
Coagulation (infrared, laser and bipolar)
Upasuaji;
Hemorrhoidectomy
Stapled hemorrhoidopexy



Njia za kuzuia Bawasiri


High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
Kunywa maji ya Uvuguvugu mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.



Kutibu kwa kutumia njia Mbadala Maradhi ya BAWASIRI:

Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine

TIBA 1: MAKAL-ARZAK

Chukua 100grm kwa kila lita moja na robo ya maji (1250ml).

Chemsha mpaka ibakie lita moja kamili.
Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha kahawa (50ml) kutwa mara tatu (1×3) mpaka dawa imalizike.

MWIKO : Mgonjwa asitumie nyama nyekundu aina yoyote,asile pili pili na wala asitumie vitu vikali.Badala yake atumie kwa wingi mboga za majani,matunda,maziwa na samaki.

TIBA 2:
Changanya unga wa Habat soda na Asali safi ya nyuki vipimo vya sawa kwa sawa.Halafu kunywa kijiko kimoja kimoja mara kwa mara.Fuatilishia na kumywa maji glasi moja (250ml) kila umalizapo kunywa hiyo dawa.

TIBA 3:
Jipake mafuta ya Mbarika kwenye utupu wa nyuma ambapo ndipo bawasiri hutokea.Fanya hivyo mara kwa mara, kwa sababu huirudisha hiyo bawasiri ndani.
Mbarika hujulikana vile vile kwa majina ya mbono,nyonyo au “castor oil”


Select Menu