News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » Video: Drake avaa wigi ili asijulikane na kuingia mtaani kuhoji watu jinsi wanavyomchukulia, wengine wampa makavu

Video: Drake avaa wigi ili asijulikane na kuingia mtaani kuhoji watu jinsi wanavyomchukulia, wengine wampa makavu

Inahitaji moyo wa ziada kuingia mtaani na kuwahoji watu wewe mwenyewe kuhusu ‘wewe’ na kisha kupata baadhi ya maoni hasi na yanayokuponda moja kwa moja kutoka kwa watu wanaodhani wanaongea na mtu mwingine.
Rapper toka Canada, Drake alikuwa sehemu ya show ya ‘Jimmy Kimmel Live’ ambapo alivaa wigi lenye ndevu za bandia ili kuficha sura yake asitambulike, na kisha kama mwandishi wa habari mcheshi akakusanya maoni ya watu katika mitaa ya Hollywood ikiwa ni sehemu ya segment ya I witness News.
Drake alikuwa anawauliza watu hao mtazamo wake kuhusu ‘Drake’ alivyohost katika tuzo za ESPY ambazo hata hivyo hazijafanyika bado.
Moja kati ya mashabiki wake ambaye hata kama hajawahi kuona maoni yake yalikuwa mazuri tu kuwa ‘aliua mbaya kwenye show hiyo’, “Drake definitely killed it’.
Lakini mwanamme mwingine alipoulizwa yeye alitoa makavu live kuwa hampendi Drake na anadhani ni muigizaji na wala sio rapper.
“I don’t like Drake, I think he’s an actor, he’s not a real rapper.” Alisema.
Wapo waliosema hawampendi na wengine wakasema sio mashabiki wake kabisa. Lakini yote aliyameza na kuendelea kuhoji tena kwa ucheshi wa hali ya juu.
Hata hivyo, alipojaribu kuwauliza itakuwaje kama akiwaambia kuwa wanaengea nae ni Drake, wengi walikuwa hawaelewi.
“I would say I’m idiot, totally idiot.”
Kijana mmoja yeye aliambiwa arap wimbo mmoja wa Drake na mwisho alikuwa surprised pale Drake alipotoa wig na ndevu za bandia na kuonesha kuwa ni yeye kweli.
Shabiki huyo alialikwa kwenye show ya Jimmy Kimmel Live akiwa na Drake.

Chanzo 100.5 Fm.


Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu