News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » » PICHA:KANYE WEST AFANYA KWELI TAMASHA LA GLASTONBURY, AVAMIWA NA NJEMBA STEJINI


 Kanye West akiwapagawisha mashabiki waliohudhuria Tamasha la Glastonbury nchini England jana usiku.
 Komediani wa Uingereza, Lee Nelson baada ya kupanda stejini kumpa sapoti Kanye West.
RAPPA wa nchini Marekani, Kanye West amefanya kweli kwa kuangusha bonge la shoo katika Tamasha la Glastonbury nchini England jana usiku.
 Mashabiki wakifuatilia burudani kutoka kwa Kanye West.
Mkali huyo alizikonga vilivyo nyoyo za mashabiki mbali na watu zaidi ya 134,000 kupinga uteuzi wa jina lake kuwemo kwenye orodha ya watu waliopanga kutumbuiza katika tamasha hilo wakitaka aondolewe na iwekwe Bendi ya Muziki wa Rock huku mwandaaji wa tamasha hilo, Emily Eavis akipokea vitisho vya kuuawa kupitia Twitter kwa uamuzi wa kumualika West.

 Mke wa Kanye, Kim Kardashian akichukua picha wakati mumewe akiwa stejini.
Shoo hiyo ya West, iliingiliwa na komediani raia wa Uingereza aitwaye Lee Nelson aliyepanda stejini kumpa sapoti staa huyo kabla ya kushushwa na wanausalama.
Kanye na Kim wakati wakiwasili Glastonbury tayari kwa shoo.

Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu