KOCHA wa Yanga, Hans van Pluijm, ameonekana kutokuwa na mzaha kwa wachezaji wote waliochelewa mazoezini bila sababu maalumu baada ya kuwapa adhabu ya kuwakimbiza ili kuwa sawa na wenzao.
Kocha huyo aliwapa adhabu hiyo Mliberia Kpah Sherman na Mbrazili Andrey Countinho ambao walichelewa kuripoti ambapo aliwasimamia kwa umakini wachezaji hao waliopaswa kukimbia kuzunguka uwanja kwa raundi 15.
Katika mazoezi hayo, kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ amezidi kupata wakati mgumu kutoka kwa kiungo Geofrey Mwashiuya kwani kila wanapokutana kiungo huyo humpigia mashuti yaliyoenda shule.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Boniphace Mkwasa alimzungumzia Lansana Kamara anayefanyiwa majaribio akisema hawawezi kutoa jibu sahihi la kumsajili mpaka watakapomtumia katika mechi kuangalia uwezo wake.
Mbali ya Kamara, alisema opia wanafikiria kumwongeza Joseph Mapembe kutoka timu yao ya vijana.
No comments