Kuna tetesi kuwa kocha mpya wa klabu ya Simba anaweza
kutokea nchini Uingereza.
Tetesi hizi za kimechezo zimedai kuwa miongoni mwa
makocha walioafanya mazungumzo ya kushika nafasi hiyo,
Muingereza huyo anaonekana kuwa kipenzi cha wana
Msimbazi.
Kutokana na kuwepo na hamu kubwa ya mashabiki kutaka
kumjua kocha wa timu hiyo, mwenyekiti wa usajili wa Simba,
Zacharia Hans Poppe amewataka kuwa wavumilivu hadi
pale taarifa rasmi itakapotolewa.
Kocha wa sasa Goran Kopunovic anadaiwa kutaka
kuongezewa maslahi zaidi ambayo Simba inayaona kuwa
makubwa mno.
No comments