News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » HUKUMU YA MRAMBA, YONA NA MGONJA YAAHIRISHWA HADI JULAI 3, 2015



Basir Mramba (kulia), Gray Mgonja (kushoto) na Daniel Yona wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
Habari: Denis Mtima na Brighton Masalu / GPL
HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basir Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona imeahirishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi Julai 3, mwaka huu.
Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya kutokuwepo Hakimu Saul Kinemela ambaye ni mmoja wa jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo. Mahakimu wengine wanaoongoza jopo hilo ni Jaji John Utamwa na Jaji Sam Rumanyika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaji John Utamwa leo ni kwamba Hakimu Kinemela yupo mkoani Dodoma kwa shughuli maalum za kibunge na anatarajia kurejea jijini Dar kati ya kesho au keshokutwa, hivyo hawawezi kutoa hukumu hiyo bila jopo hilo kukamilika. GPL

Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu