BARCELONA majanga yanaendelea, ilitamba na pasi zake uwanjani, lakini ikashindwa kuwapa raha mashabiki wake baada ya kuchapwa na mahasimu wao Real Madrid mabao 2-1 kwenye fainali ya Kombe la Mfalme iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mestalla mjini Valencia, Hispania jana Jumatano usiku.
Staa ghali duniani, Gareth Bale alifunga bao safi la jitihada binafsi kuipa Real Madrid ushindi safi kwenye El Clasico hiyo ya tatu msimu huu na kuiwezesha timu yake kutwaa taji la kwanza kubwa msimu huu baada ya kumzidi mbio beki wa Barcelona, Marc Bartra na kufunga kwenye dakika 85.
Staa wa Argentina, Angel Di Maria alikuwa wa kwanza kuifungia bao la kuongeza Real Madrid kwenye dakika ya 11, kabla ya Barcelona kusawazisha dakika 68 kupitia beki wake wa kati, Bartra.
Barca nusura isiwazishe, lakini shuti la Neymar liliishia kugomba mwamba na kipa Iker Casillas kufanikiwa kuudaka mpira huo.
Video ya magoli iko hapa Chini.
No comments