News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » Q Chief alimuomba msamaha Juma Nature baada ya kushiriki kwenye wimbo wa wanaume Family 'Kazi Ipo', asema Said Fella hakumbuki...

Q Chief alimuomba msamaha Juma Nature baada ya kushiriki kwenye wimbo wa wanaume Family

Miaka kadhaa iliyopita ngome ya ‘Wanaume TMK’ ilipata mpasuko na baadhi ya wasanii wakiongozwa na Juma Nature walijiondoa kwenye uongozi wa Said Fella na kuunda kundi la Wanaume Halisi.
Mgawanyiko huo haukuwa wa maridhiano ya amani na baadae makundi hayo yalirushiana makombora kwenye nyimbo zao, Wanaume Halisi wakitoa wimbo unaoitwa ‘Ndege Tunduni’ na wale waliobaki wakitoa ‘Kazi Ipo’ waliomshirikisha Q Chief au Q Chilla kama anavyojiita hivi sasa.
Q Chief ameiambia The Jump Off ya 100.5 Times kuwa kujihusisha kwenye wimbo huo kulimpa lawama kubwa kuliko lawama zozote ambazo aliwahi kuzipata katika muziki kutoka kwa mashabiki wengi waliomsapoti Juma Kassim Nature.
“Nataka nikuambie kitu kimoja, katika lawama ambayo niliwahi kuingia katika maisha yangu ni lawama ya kumsapoti Fella na kumuacha Juma kwa sababu watu wengi walikuwa wakimpenda Juma…umenielewa. Lakini kinachonisikitisha ni kwamba hilo Fella hii leo halioni kwamba I risked my life for him. Nikamuacha Juma na kumsapoti yeye.” Q Chilla alimwambia Jabir Saleh mtangazaji wa The Jump Off.
Ameeleza kuwa baadae ilibidi amfuate Juma Nature na kumuomba msamaha baada ya kuhisi hakufanya uamuzi sahihi.
“Nilivyovuta memory yangu nyuma nikasema nahitaji kumuomba msamaha Juma hata kama ilikuwa ni game na nilimfuata mpaka Temeke. Nikamwambia brother mimi naomba radhi, najua mambo mengi labda yalisimama kwa namna moja ama nyingine lakini sitaki kumlaumu mtu yeyote. Tumepitia mengi tuendelee. Lakini sijui kama Fella atakumbuka hili, kwa roho moja nalitoa moyoni.” Ameongeza.
Alipoulizwa kama aliwahi kumfuata pia Fella kama alivyomfuata Juma Nature:
I don’t need to check Fella, he needs to check me. It doesn’t matter if he is a boss or something.. I risked my life for Fella and then what did he pay me? He just left me kama vile nimeshamaliza! Hakujali wala kujua Mungu anapanga vitu kwa makusudi. Simzungumzii vibaya…sio mtu mbaya, nataka akumbuke kitu gani aliwahi kufanyiwa nikiwa hai sio mpaka siku nimekufa aseme nilishawahi kufanya hiki na hiki. Watoto wa kiume ni watoto wa kiumeni. Fella anatakiwa kuwa mwanaume zaidi (hahaaa)…you know what I mean.
The Jump Off ya 100.5 Times Fm inakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili kamili usiku hadi saa nne kamili. Unaweza kusikiliza kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliandikwa ‘Listen’.
Chanzo 100.5 fm.




Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu