News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » Kanye West na Kim Kardashian kufunga ndoa ya serikali wiki hii



Kanye West and Kim Kardashian wako tayari kufanya mahusiano yao kuwa rasmi kisheria ambapo wiki hii watafunga ndoa ya kiserikali.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ wawili hao wamepanga kufunga ndoa ya kisheria wiki hii kimya kimya bila ya kuwa na watu wengi.
Sherehe rasmi za ndoa hiyo zinatarajia kufanyika Paris Ufaransa mwezi ujao na inatarajiwa kuhudhuriwa na watu wengi maarufu.
Hii itakuwa ndoa ya kwanza kwa Kanye na ya tatu kwa Kim K.
Mara ya kwanza Kim aliolewa mwaka 2000 akiwa na miaka 20 na mtayarishaji wa muziki Damon Thomas lakini ndoa hiyo ilidumu kwa miaka minne. Mwaka 2011 alifunga ndoa na mchezaji wa mpira wa kikapu, Kris Humphries ambaye waliachana rasmi mwaka 2013.

Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu