News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » HUYU NDIE MWANAUME ALIYEJIZIKA KUKWEPA MATATIZO YA NDOA.


Matumaini aliyosalia nayo mwanamume huyo ni ya kwenda mbinguni
Mwanamume mmoja nchini Kenya aliwaacha wakazi wa kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni matatizo ya ndoa.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift Valley


Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndhio maana akaamua kujitoa uhai.Mwanamume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.

Mwanamume huyo kwa jina Kipsang , alichimba kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wanalala.
Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumwba na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.
Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya Ndizi neneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.


Chanzo BBC

Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu