News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » » Wahdzabe wataka kutambulika kwenye Katiba

JAMII ya kabila la Wahadzabe waishio katika kijiji cha Olpiro kata mpya ya Eyasi Wilayani Ngorongoro, wameiomba serikali kutunga sheria kupitia katiba mpya Pendekezwa zitakazolinda na kutambua uwepo wao na maslahi yao katika maeneo wanayoishi


Vijana wakihadzabe wakiwa mawindoni
Wito huo wameutoa jana kijijini hapo, katika semina maalum ya elimu ya uraia kufahamishwa kilichomo ndani ya katiba pendekezwa iliyokuwa ikiendeshwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Pingo’s Forum, ili kuwaandaa kabla ya kura ya kupitisha katiba hiyo.

Akizungumza katika semina hiyo, Matayo Gudunarya wa kabila la kihadzabe amesema jamii hiyo ndogo katika eneo hilo, hivi sasa wanaishi zaidi ya ukimbizi kutokana na maeneo yao wanayotegemea kupatia riziki kupewa wawekezaji na wao kubaki katika hali ngumu ya maisha.
Naye Hamisi Saliboko akiongelea suala la maslahi yao kama Wahadzabe kuingizwa katika katiba hiyo, amesema alitegemea katiba mpya itatoa ruhusa kwao kama watumiaji matunda ,urinaji wa asali na wanyama pori wadogo, kuruhusiwa kufanya shughuli hizo katika eneo lolote jirani na makazi yao ama kutengewa eneo maalum.

Akitoa mfano amesema katika kijiji chote hicho wapo 29 tu kwa muda yote hawaongezeki kutokana na ukosefu wa upatikanaji wa vyakula vya asili, kwani wanabanwa kila upande ambapo upande mmoja yupo muwekezaji wa kampuni ya Mwiba huku kwingine ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Amesema kutokana na hali hiyo wakati mwingine ili waweze kuendelea kuishi wanalazimika kuingia porini pembezoni mwa hifadhi kuwinda wanyama wadogo ili kujipatia riziki.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Gabrieli Lokhai, akiongelea jamii hiyo, amesema wamekuwa wakiishi nao kijijini hapo lakini kwa muda mwingi wahadzabe hao huwa katika mapori ya pembezoni mwa kijiji hicho.

Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu