Je unajua kuna ugonjwa ambao tiba yake ni kula kinyesi? NDIO unakula mavi yaani choo cha binadamu.
Ugonjwa huo unaitwa ulcerative colitis unasababishwa na bacteria C.difficile. Ni ugonjwa ambao unakufanya unaharisha sana, yaani siajabu kuhara hata mara arobaini kwa siku. Bila tiba unaweza kupoteza maisha yako.
Kwenye utumbo mkubwa kuna bacteria wazuri na bacteria wabaya. Ugonjwa huu husababishwa na utumiaji wa hovyo wa dawa kali za antibiotics kwa kipindi kirefu ambazo huua wadudu wazuri na kufanya wadudu wabaya kuongezeka na hatimaye kuleta madhara ya kuhara sana.
Swali linakuja... ugonjwa unaosababishwa na kutumia dawa za antibiotics je utawezaje kutibiwa na dawa hizo hizo?
Kuna tiba gani ambayo itaua wadudu wabaya kwenye utumbo bila kudhuru wadudu wazuri?
Jibu ambalo sisi madaktari tulipata ni kumpa mtu kinyesi cha binadamu mwenzie, yaani kinyesi chenye bacteria/wadudu WAZURI wakutosha. Anaejitolea kinyesi chake kwanza hupimwa kukakikisha hana magonjwa kama hiv, hepatitis nk. Hupewa dawa ili apate choo siku hio, kinyesi huchukuliwa na kusagwa kwenye blender, alafu mgonjwa hupewa kwa njia ya mrija puani au mrija kwenye tundu la haja kubwa.
Niambie kama ni wewe uko tayari 'kula' kinyesi kuokoa maisha yako?
Je uko tayari kumpa ndugu yako, mke/mume wako choo chako akile?
No comments