KWANZA kabisa inabidi tujue kinachosababisha mwanamke asipate mimba au watu wengine huita ugumba.
Ugumba ni ile hali ya mwanamke kupoteza uwezo wa kubeba mimba au mwanaume kushindwa kusababisha ujauzito.
Ugumba ni ile hali ya mwanamke kupoteza uwezo wa kubeba mimba au mwanaume kushindwa kusababisha ujauzito.
Na kwa mwanamke hali hii hutokea pale anaposhindwa kubeba ujauzito na hii inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama kuvurugika kwa homoni, uvimbe katika kizazi, maambukizi ya aina mbalimbali kwenye kizazi cha mwanamke na mambo mengine mengi kama nitakavyoyaelezea hapo baadaye.
Kwa upande wa mwanaume tunasema anashindwa kusababisha ujauzito kwa mwanamke kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuwa na mbegu zisizokuwa na nguvu ya kutosha au kuwa na mbegu chache kabisa.
AINA ZA UGUMBA
Kwanza kuna aina ya ugumba inaitwa kitaalamu Primary Infertility; hii ni aina ya kwanza ya ugumba ambayo yenyewe inawahusisha sana wanawake ambao hawajawahi kuzaa hata mara moja, na wanakutwa na hii hali ya kutokubeba ujauzito.

Pili, kuna aina inayoitwa Secondary Infertility: Hii ni ile hali ambayo inampata mwanamke lakini baada ya kubeba ujauzito na kuzaa au kutokuzaa kwa mara ya kwanza na baadaye akapatwa na hali ya kutokubeba ujauzito.
Watafiti wanasema kuwa tatizo hili la ugumba limekuwa ni sawasawa kwa jinsia zote mbili, kwa maana kwamba wanaume nao wana uwezekano uleule kama walionao wanawake wa kuwa na tatizo hili la ugumba.
Ni vizuri kujua kwamba si wanawake tu ndiyo wanaweza kukumbwa na tatizo hili bali hata wanaume nao wanaweza kukumbwa na tatizo hili.
Ni vizuri kujua kwamba si wanawake tu ndiyo wanaweza kukumbwa na tatizo hili bali hata wanaume nao wanaweza kukumbwa na tatizo hili.
DALILI ZA UGUMBA
Kwa tatizo hili ningependa kugawanya dalili hizi za ugumba katika makundi mawili ili tuweze kuelewana kwa urahisi zaidi juu ya tatizo hili.
Kwa tatizo hili ningependa kugawanya dalili hizi za ugumba katika makundi mawili ili tuweze kuelewana kwa urahisi zaidi juu ya tatizo hili.
Dalili zipo nyingi kama vile mwanamke kukosa hedhi au kupata matatizo ya hedhi, hasa kwa wanawake ambao hedhi zao hazina tarehe maalumu.
Wengine wana tatizo la hedhi kukoma na wakati umri bado haujafika, hedhi nyingi kupita kiasi, hedhi ndogo kupita kiasi na matatizo yote yanayohusisha hedhi kwa mwanamke yanapaswa kuchunguzwa na daktari.
Dalili nyingine kwa wanawake ni ile hali ya kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya na rangi ya kahawia sehemu za siri, hili ni tatizo zito na kubwa sana kwa wanawake.
No comments