Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Chacha Mwita (24) amekufa baada ya kuchomwa kisu na mwenzake wakigombea mwanamke.
Imeelezwa kuwa siku ya tukio marehemu akiwa kwenye baa
moja mjini Sirari, nyakati za jioni kulitokea ugomvi kati yake
na mtu mwingine ambaye hakufahamika jina wakigombania
mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Dina. Wakati wa
ugomvi huo, Mwita alichomwa kisu kifuani na aliyefanya
kitendo hicho alitoroka ambapo majeruhi huyo alitokwa
damu nyingi na alipofikishwa Hospitali ya Wilaya Tarime
alifariki dunia.
No comments