News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » Simba yaongeza beki Mrundi kikosini


SIMBA ipo katika hatua za mwishoni za kumsainisha beki wa pembeni kutoka Vital’O ya Burundi, lakini wanafanya siri kubwa mpaka itakapomshusha Dar es Salaam kushangaza mashabiki wake.
Beki huyo anayecheza namba mbili na tatu yupo katika mazungumzo nao na imeelezwa kuwa endapo Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) litatangaza rasmi kuruhusu wachezaji saba wa kigeni, basi beki huyo atatua nchini dakika yoyote.
Mpaka sasa Simba imesajili wachezaji wapya sita ambao ni Laudit Mavugo wa Burundi, Musa Mgosi aliyekuwa anakipiga Mtibwa Sugar, Peter Mwalyanzi kutoka Mbeya City, Samir Haji Nuhu, Mohammed Fakhi kutoka JKT Ruvu na Mohammed Abdulrahman aliyetokea JKU.
Simba inamsainisha mchezaji huyo ili kuwaongezea presha ya ushindani Hassan Kessy na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambao wanaonekana kutokuwa na changamoto. Nafasi nyingine watakayoongeza mchezaji ni mshambuliaji.
Tayari Simba imefikisha wachezaji watano wa kigeni wanaoruhusiwa sasa. Hao ni Emmanuel Okwi, Juuko Murshid, Simon Sserunkuma na Laudit Mavugo.
Chanzo Mwanaspot

Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu