News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » » Huyu ndiye Bilionea Masarufu anaye mmiliki Muimbaji maarufu MARIA CAREY

Nyota wa R&B, Maria Carey akiwa na  bilionea, James Packer.
CANNES, Ufaransa
HISIA ni kitu kingine! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya nyota wa R&B, Maria Carey, 45, kunasa katika penzi la bilionea, James Packer, 47, raia wa Australia.
 Maria, aliwahi kuolewa na Nick Cannon lakini waliachana Agosti mwaka jana kwa talaka baada ya kudumu kwenye uhusiano kwa miaka sita wakiwa na watoto wawili mapacha.
Taarifa ni kwamba hivi sasa mwanamama huyo mrembo amenasa kwenye penzi la bilionea huyo kijana. Imeripotiwa kuwa, Maria na James wamekuwa karibu na wamekuwa wakionekana pamoja wakila raha huku wakionekana sehemu mbalimbali kama Casino, migahawani na kwenye boti wakiwa wameshikana mikono kimahaba.
 Bilionea huyo ameripotiwa na Jarida la Forbes kuwa anashika namba nne kwa utajiri nchini Australia.

Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu