News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » Mfungwa awashitaki Jay Z, Beyonce, Kanye West, Chris Brown na Rihanna, adai walimuibia nyimbo 3,000, ataka fidia $ bilioni 2


Katika hali isiyo ya kawaida, polisi wa California wamepokea mashitaka toka kwa mfungwa mmoja akiwashitaka wanamuziki wakubwa wa hip hop, na R&B akiwadai fidia ya $ bilioni 2.
Katika faili la kesi hiyo, mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Richard Dupree amewataja Beyonce, Jay Z, Kanye West, Rihanna na Chris Brown kuwa walimuibia mashairi ya nyimbo zake 3,000 alizoandika wakati akiwa gerezani.
Kwa mujibu wa huffingtonpost, Dupree alifungua mashitaka katika mahakama ya wilaya ya mashariki mwa California April 21, na anaamini kuwa Beyonce na Jay Z walifanya kazi na CIA, FBI na vitengo vingine vya ulinzi wa Marekani kumpeleleza na kuyapata mashairi yake.
Anaamini kuwa Chris Brown, Kanye West na Rihanna walihusika na ku-organize kundi la watu waliomuibia mashairi ya nyimbo hizo 3,000.
Habari hii ya kweli inaweza kuchukuliwa kama sehemu ya ucheshi kwa wote waliotajwa lakini Dupree yuko serious.








Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu