Ubunifu: Miaka 50 Ya Muungano wa Tanzania, Washington DC. |
 |
Mhe. Mwigulu Nchemba akikata utepe kuashiria kuwa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano, Washington DC zimefunguliwa rasmi. Kulia kwake ni Balozi Liberata Mulamula na kushoto kwake ni Waziri anayeshughulikia Muungano-Zanzibar, Mhe. Mwinyihaji Makame. |

Mh. Nchemba akiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Bi. Mulamula kuelekea kufungua sherehe hizo.
Mke wa Mhe. Nchemba (kulia)akisalimiana na mwanamitindo wa mavazi, Miss Temeke wa "KWETU FASHION".
Nchemba akitembelea mabanda ya maonesho ya vitu mbalimbali vya asili ya Tanzania nje ya Jengo la Ubalozi wa Tanzania, Wahsington DC.
Nchemba akipata maelezo kuhusu vitenge na khanga zilizotengenezwa Tanzania, zinazouzwa nje ya Jengo la Ubalozi.
Viongozi wakionja chakula cha asili cha Tanzania kilichopikwa Washington DC: Ugali wa mhogo, Makande, Ndizi, Kisamvu n.k vilikuwepo.
Katikati ni Bwana Okoka Sanga akiwa na viongozi wa Kitaifa waliofika kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. Okoka Sanga ni mtengenezaji wa kadi na mifuko ya zawadi jijini Washington DC.
Bidhaa za Bakharesa pia zilikuwepo.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi. Kutoka Huston-Texas waliofika hapa Washington DC wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Mwigulu Nchemba mara baada ya kuzungumza machache kuhusu kuimarisha Chama, Marekani,
Mhe. Nchemba akimvisha skafu ya Tanzania huyu mtoto wa Kizulu (Afrika Kusini) aliyepiga ngoma na kufanya umati ushangilie kwa shangwe. Baba yake aliwahi kuishi Tanzania mwaka 1982.
Kikundi cha wacheza ngoma ya asili cha Watanzania waishio hapa Marekani kikitumbuiza.
 |
Kwetu Fashion |
Nje ya Jengo la Ubalozi Watanzania wanabadilishana mawazo.
Mtanzania akiwaongoza wazungu hawa kula moja ya vyakula vya asili vya Tanzania.
Miss Tanzania wa hapa Marekani aliyeshinda mwaka 2013/2014 akiwasili Ubalozini tayari kwa kuungana na Watanzania kusherekea Miaka 50 ya Muungano.
Mtoto akionesha uwezo wa kucheza ngoma ya asili.
Chombo cha habari "SAUTI YA AMERIKA" nao walijumuika. Mtagazaji Hamza Mwamoyo akiwa na viongozi wa Serikali ya Tanzania Mh:Mwigulu NChemba (Kulia) na Mhe. Mwinyihaji (kushoto) baada ya kufanya kipindi kitakachorushwa na idhaa ya Kiswahili ya redi hiyo.
Col. Mutta (kulia) wa Ubaliozi wa Tanzania akimkaribisha kiongozi kutoka Ubalozi wa Cameroon hapa Washington DC.
Mapokezi yanaendelea kwa wageni kutoka Mataifa mbalimbali waliohudhuria.
Askari wa mataifa mbalimbali waliojumuika na Watanzania. Kutoka kushoto ni Mabalozi wa Nigeria, Poland, Zimbabwe na Zambia pamoja na Mwigulu Nchemba.
Kushoto ni ndugu Mrisho Mzese kutoka Maryland. Ndiye Mwenyekiti wa Shina la CCM
Watanzania katika mavazi ya Kiafrika
Kushoto ni Raia wa Nigeria na kulia ni Raia wa Cameroon.
Nchemba akibadilishana mawazo na Wazungu waliowahi kuishi Tanzania miaka ya 1990.

Dada wa Kitanzania aliyesafiri Kutoka Calfonia hadi Washington kwa ajili ya kuongoza Watanzania kuimba Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Marekani. Ameonesha Kipaji chake cha kuimba nyimbo zote mbili kwa ustadi mkubwa.
Balozi Libereta Mulamula akiwa na mumewe alipomuita kwa ajili ya kumtambulisha kwa Watanzania waliofika kusherekea Miaka 50 ya Muungano.
Viongozi wakisikiliza kwa makini maneno ya Balozi Mulamula.
Mmoja ya Viongozi wa Serikali ya Marekani akifurahia umoja na urafiki wa Tanzania na Marekani kidiplomasia. Ameomba uendelee kudumishwa.
Mhe. Mwinyihaji Makame akizungumzia umuhimu wa Muungano kwa Wazanzibari. Amesisitiza Watanzania wajikite kujadili maswala ya maendeleo badala ya kuoongeza idadi ya Serikali.
Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano.
Nchema amesema ni wajibu kwa kila mmoja wetu katika kizazi hiki kuandika historia ya kipekee kwa kuulinda na kuudumisha Muungano wetu kwa Miaka 50 zaidi. Kizazi kijacho kitawahukumu Watanzania endapo Muungano utavunjika kwa sababu tu ya kupenda vyeo na ukosefu wa utashi wa kisiasa.
Mwigulu na Mke wake (kushoto).
Viongozi wa Chama Cha mapinduzi Kutokea Texas.
MC akiendesha Shughuli kwenye Usiku wa Miaka 50 ya Muungano.
Viongozi wa mataifa mbalimbali katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Nchemba na MwinyihajimMara baada ya Nchemba kuzungumza na Watanzania.
Usiku wa Muungano ulipambwa na nyimbo za Kitanzania tu. Hapa muziki unaendelea.
Mhe. Mwigulu Nchemba akizunguma na Watanzania Kwenye Usiku wa Miaka 50 ya Muungano hapa Washington DC.
Mwigulu alizungumzia kuhusu suala la uraia-pacha na kuwaahidi Watanzania kuungana nao katika kuipata haki hiyo Kikatiba.
Alisema Chama cha Mapinduzi kimependekeza hilo kwenye Rasimu ya Katiba Mpya. Pia amezungumzia sababu za kiuchumi kuhusu mzigo wa Serikali ya tatu inayopendekezwa na Rasimu huku akiwapa uhuru Watanzania kutafakari kwa kina kuhusu hilo.
Mwishowe alizungumzia kuhudu dhamira ya wazi ya UKAWA (Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi) kuvuruga mchakato wa Katiba kwa kusema kuwa dhamira hiyo imepangwa kutoa awali wakati wa ukusanyaji wa maoni na hata kwenye uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Akasema, hivyo kususia kwao Bunge ni jambo walilopanga na wamelitekeleza.
Mwigulu amepeleka pongezi kwa Watanzania wote waliopuuzia kitendo hicho walichokifanya UKAWA kwa kusema hakikuwa cha kizalendo na kilicholenga kuligawa Taifa.
No comments