News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » Tunaomba radhi kwa picha: Hizi ni picha 11 za Mauaji yaliyofanyika sudani kusini.

 Umoja wa Mataifa unasema kuwa vikosi vinavyoipinga serikali nchini Sudan Kusini viliwaua mamia ya watu kwa sababu ya kabila lao wakati vilipouteka mji wa Bentiu wiki jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, watu hao walilengwa wakiwa katika maeneo salama walikokuwa wanahifadhiwa kama vile msikitini, makanisani na hospitalini.


Watu wa kabila laNuer, ni wafuasi wakubwa wa kiongozi wa waasi na makamu wa zamani wa Rais Riek MacharUmoja huo umesema kuwa watangazji katika baadhi ya vituo vya redio walitumia lugha ya chuki na uchochezi na kuwataka watu wa kabila fulani kuondoka mjini humo huku wakiwashauri wanaume kuwabaka wanawake.

Wapiganaji wanaomuunga mkono makamu wa rais wa zamani Riek Machar waliuteka mji wa Bentiu ambao ni mji mkuu wa jimbo la Unity siku sita zilizopita.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walilaani kile walichokitaja kama mauaji yanayowalenga raia kwa misingi ya ukabila.
Rais Salva Kiir anatoka kabila la Dinka ambalo ndilo kabila kubwa kuliko yote nchini Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu ambao hawakuwa wa kabila la Nuer,waliuawa Bentiu.
















Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu