
Meli ya Korea Kusini iliyokuwa imewabeba zaidi ya abiria mianne ilizama kusini mwa pwani ya nchi hiyo Jumatano asubuhi

Walioshuhudia ajali walisema kuwa walisikia kishindo kikubwa wakati meli hiyo ilipoanza kuzama

Wanafunzi wengi waliokolewa kupitia mashimo yaliyo kando ya meli hiyo huku wengine wakiruka baharini katika jitihada za kuokoa maisha yao

Wazazi, jamaa na marafiki wa wanafunzi waliokuwa katyika meli hiyo wanatizama kupitia televisheni picha za meli hiyo ilipozama

Inaarifiwa zaidi ya watu miatatu hawajapatikana , wengine 164 waliweza kuokolewa na watu wawili wamethibitishwa kufariki

Watu wawili wameripotiwa kufariki ingawa shughuli ya uokozi ingali inaendelea. Wengine zaidi ya miatatu bado hawajulikani waliko

Wengi wa watu waliokuwa katika meli hiyo walikuwa wanafunzi waliokuwa katika ziara ya kisiwa kimoja nchini humo
No comments