Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limezima mitambo miwili ya uzalishaji maji kwenye mitambo yake ya Ruvu Juu uliopo Mlandizi, mkoani Pwani na Mtoni uliopo Temeke, Dar es Salaam.
Hatua ya DAWASCO imetokana na mvua kubwa zilizonyesha kusababisha madhara mbalimbali katika miji ya Kibaha, Pwani na Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ilieleza kutokana na sababu hizo maeneo yatakayokosa huduma ya maji ni Kijichi, Mbagala Zakheam, Mtoni kwa Azizi Ally, kwa Kabuma, Azimio Kaskazini na Kusini, Wailes, Mwembe-Yanga, Sudan, Mivinjeni na Mtoni Sabasaba. Maeneo mengine ni Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Chuo Kikuu, Kibangu, Riverside, Barabara ya Mandela, Tabata na Segerea.
“DAWASCO inawaomba wananchi radhi kwa usumbufu utakaojitokeza … kazi itaanza baada ya mafuriko kupungua Ruvu Darajani na Mto Kizinga,” ilieleza taarifa hiyo. ---
Tanzania Daima
No comments