News

Music

Makala

Sokkaa

Video

» » » MGENI KARIBU MWENYEJI APONE

Mmoja wa wafanyabiashara Jijini Arusha Leo wakiwa wanauza 
Jezi na vifaa vingine vya michezo kwa ajili ya kesho katika uwanja Sheikh Amriabeid.
Picha na John Msinini.




Mgeni njoo mwenyeji apone!!! Huu ni usemi ambao umekuwa ukitumika sana na watu ukiwa unamaanisha anapokuja mgeni kwako lazima utamwandalia na katika kuwandalia Sio kwamba vile unavyoandaa atavifaidi yeye peke yake lahasha wote mtakuwa mnavifaidi.
Nazani pia huu msemo si vibaya tukiutumia hata kwenye soka ila kwenye soka iko tofauti kidogo kwani hii hutokea kwenye maandalizi ya mashindano au mechi husika mfano mzuri ni kule South Africa ambapo yalifanyika mashindano ya kombela Dunia mwaka 2010,South Africa walipata nafasi ya kuandaa mashindano yale lajini pamoja na kuyaanda walipata faida kubwa kutokana na wageni waliokuwa wamekuja kwaajiliya mashindano hayohivyo biashara mbalimbali zilipata mafanikio kutokana na ujio ule wa wageni waliokuwa wamekuja kushiriki na kushuhudia michuano ile. Hivyohivyo kwa michuano inayotegemewa kufanyika siku za hivi karibuni kule nchini Brazili, Brazili nao wamepata nafasi yakuanda michuano hiyo kitu ambacho kitawafanya kupata mafanikio pindi timu zitakapokuja na wale wanokuja kushuhudia michuano hiyo hapa ndipo unapokuja huu msemo wa ''Mgeni njoo mwenyeji apone''

Tuachane na huko Brazili turudi hapa kwetu Tanzania, Imekuwa kama ni kawaida kwa kila mkoa inapofanyika michuano mikubwa hasa kwa upande wa ligikuu mkoa ambao kunakuwa na mechi kubwa kama za Simba,Yanga,Azam,Mbeya city kuwa ni kama fursa kwa wafanya biashara kufanya biashara zao vizuri na kupata wateja wengi kutokana nakuwa wenyeji mfano kesho Arusha ni mwenyeji wa mchezo wa Yanga dhidi ya JKT Oljoro  hivyo inakuwa ni kama fursa kwani wafanya biashara wa vitu kama Jezi za club,kofia,bendera,na hata mavuvuzela wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa mafanikio kwani wanakuwa na wateja wakutosha.
Swali langu linakuwa ni Je? sisi kama wafanyabiashara tunazipa timuzetu za mikoani ushirikiano wa kutosha au Tunakuwa tukizishangilia timu zinazokuja Ili msimu unaokuja tuweze kufaidika na ujio wao kushindana na timu yetu tena? Hapa nazani jibu ni hapana ila kwa timu kama Mbeya City wameonyesha mfano mzuri kwani hatakama ni shabiki wa Yanga linapokuja swala la Timu ya mkoa wake huwa wanaiacha Yanga na kuishangilia Timu yao ya Mbeya City. Kwa mikoa kama Arusha,Tabora sidhani kama wataweza kufaidika na wageni kwa msimu unaokuja kwani wameshindwa kuzipa Suport hivyo kusababisha kuwa na hali ngumu kuelekea kushuka Daraja. Chakufanya ni kuwa wazalendo na timu za mikoa yetu na huwa siku zote uzalendo unatokea sehemu unapotokea endapo utashindwa kuwa mzalendo kwa kuishangilia timu ya mkoa unapotoka au wilaya ni dhahiri kuwa hata uzalendo wa taifa lako utakuwa mgumu. TUBADILIKE,
Na Rajab Makenda.

Mwananchi Kweli

Tunakushukuru kwa kuendelea kusoma habari zetu tunakuomba kama unapatwa na tatizo lolote hapa kwenye tovuti yetu una maoni,Habari na ushauri usisite kutuandikia kwenye info@news4timeblog.com kisha tutakujibu haraka iwezekanavyo.Hasante.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply

Select Menu