Kwa mara ya kwanza hoteli maarufu duniani ya Hyatt Regency ya Hong Kong imetoa simu aina ya smartphone bure kwa wageni wake waliopanga kwenye hoteli hiyo.
Hoteli hiyo ya Hyatt Regency pia ilitoa viburutisho mbalimbali kama vile chocolates na mvinyo wa bure pamoja na simu aina ya smartphone katika vyumba vyake vyote 381 ili jitihada za kuongeza uzoefu kwa wasafiri na watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Katika kuwapa smartphone wateja wake za bure ni katika kutoa wito na juhudi za kibiashara na kutafuta masoko mapya ndani na nje ya Hong Kong hasa wageni kutoka Marekani, Uingereza, Australia, Singapore na China.
Simu hizo aina 3G zenye intaneti, maingiliano ya ramani na vitu kadhaa za kufurahisha mtumiaji na kuboresha huduma yake ya mawasiliano wakati wote.
Simu hiyo ya smartphone inatoa mambo mengi kama vile namba za dharura, chaguzi za usafiri mbalimbali, aina ya maduka, migahawa vile vile miji maarufu na mitandao ya Facebook, Instagram, skype na mitandao mingine ya habari ya kijamii.
Aina hiyo ya simu ya smartphone unaweza kununua hata kwenye hoteli kwa dola za kimarekani USD 250 tu.
No comments