
Habari za kusikitisha kutoka Kijiji cha Ng'ereng'ere Kata ya Nyamaraga wilayani Tarime katika Mkoa wa Mara zinasema mkazi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Michael Bokoyo (64) anatuhumiwa kumuua binti yake mwenye umri wa miaka 10 kwa mpini wa jembe akimtuhumu kupalilia shamba vibaya.
Gazeti la HabariLeo linataarifu kuwa mtoto aliyeuawa ni Neema Michael aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Ng'ereng'ere kwa kumpiga na mpini akimtuhumu wa kuacha magugu shambani.
Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Justus Kamugisha amekaririwa na gazeti hilo akisema kuwa tukio hilo ni
la Aprili 17 mwaka huu, kwamba, baba huyo mzazi alikwenda kukagua shamba lake la mahindi ambalo watoto wake walikuwa wakipalilia na alipokuta nyasi ambazo Neema hakuzing'oa, ndipo alimnyang'anya jembe na kumpiga nalo kichwani upande wa jicho la kulia.
Imeelezwa kuwa marehemu mtoto huyo alipata jeraha kubwa lililotoa damu. Inadaiwa baba yake aligoma kumpeleka hospitali na kesho yake, Aprili 18 mtoto huyo alifariki dunia.
Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.
No comments