Hii ilitokea siku ya jumapili kwenye mechi kati ya Barcelona Vs Villareal ambayo Barcelona ilishinda kwa magoli 3-2. Mkasa huo ulitokea wakati mchezaji wa Barcelona Dany Alves alipokuwa ana piga kona ndipo mashabiki wa Villareal walipo mrushia ndizi na kwakuonyesha kuwa mchezaji huyo hakujali kabla yakupiga ile kona aliichukua ile ndizi nakuimenya kisha akaila nusu na kipande kingine akikirusha pembeni ya uwanja.
Alipohojiwa alisema '' Naona kawaida kwani nimeishi hapa Hispania kwa zaidi ya miaka 10 ni vitu kama hivi vimekuwa vikifanywa hata kwa wachezaji wenzangu na mimi naamini wote ni Nyani'' alisema alves.
Dany Alves mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na club ya Barcelona Mwaka 2008 kwa ada ya kitita cha paundi 23m. Amekuwa akipinga vitendo vya kibaguzi kwa mashabiki wa Hispania kwa muda mrefu jambo ambalo hata Fifa wamekuwa wakilipinga kwani kumekuwa na ubaguzi wa watu wenye asili ya Africa wanapokuwa wakicheza katika ligi hiyo.
Baada ya Alves kufanya kitendo hicho wamejitokeza wacezaji wengine kumuunga mkono kwa kupinga ubaguzi nakusibitisha kuwa wote ni nyani kwa kupost picha kwenye mitandao ya kijamii wakila ndizi. wachezajio hao ni kama Sergio Aguero, David Luiz, Oscar, Willian, Nacer Chadli and Moussa Dembele
Hapo chini ni picha walizo post
Star wa Chelsea Oscar,David Luiz na William kwapamoja wakimuunga mkono.
Kulia ni kinda wa Brazili na Barcelona na kulia mchumba wake Dany Alves wote walipost picha zao kwenye mtandao wa Instagram wakionyesha Suport kwa Alves.
Sergio Aguero na Marta
Television presenter Marilo Montero
Wachezaji wa Totenham Mousa Dembele na Nacer Chadli
Philippe Coutinho na Luis Suarez
Wakati akila ndizi iliyorushwa
Macherano akimkumbatia Alves kuonyesha umoja
Hapo chini ni Video ya tukio
No comments